Magufuli amtaka Kigogo huyu kustaafu kwa Hiari yake

Wimulehope 2017-10-31

Views 2

Rais John Magufuli amemtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasa) Archado Mtalemwa ajiandae kustaafu kutokana na mapungufu mengi ambayo Rais amesema ameyaona katika mamlaka hiyo.\r
Rais ameyasema hayo leo(Jumatano) akiwa katika ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani na alitumia fursa hiyo kuzungumzia miradi ya maji na ulipaji wa maji kwa taasisi za serikali.\r
“Ndugu yangu Mtalemwa, naongea kwa lugha nzuri hapa, nikuombe tu kuwa ustaafu mapema, inawezekana Waziri wa Maji ni rafiki yako, kama ilivyo kwa mawaziri wengine, lakini nadhani huu ni wakati mzuri,” amesema na kuongeza;\r
“Pamoja na kazi zako nzuri, its your time to go.”\r
Rais Magufuli amezungumzia kero mbalimbali za maji na kusema kuna upotevu mkubwa wa maji.\r
\r
Subscribe Our Channel: \r
\r
Follow and Like Us On Facebook:

Share This Video


Download

  
Report form