Kikosi cha Asante Kotoko kimewasili saa 3 asubuhi ya leo tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba SC utakaopigwa kesho kwenye dimba la Taifa Dar es Salaam katika Tamasha la Simba Day 2018
Kocha wa timu hiyo, pamoja na Nahodha wa kikosi wamesema wamejipanga kuipa kutandaza soka la kiwango cha juu huku Kaimu Makamu wa Rais wa Simba Idd Kajuna akiwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye tamasha hilo.