Manara :Simba Musishangilie Okwi Akifunga Goli Kwasababu hii Hapa

Popular Video en 2018-09-07

Views 2

Uongozi wa klabu ya Simba umewataka mashabiki wake na watanzania kwa ujumla kuipa sapoti Taifa Stars ambayo inacheza kesho dhidi ya Uganda kuwania tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON 2019.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, amesema watanzania wote wanapaswa kuwa kitu kimoja kwa kuonesha utaifa na uzalendo kwa Stars ambayo itakuwa inaiwakilisha nchi.

Aidha, Manara amesema atawashangaa mashabiki baadhi wa Simba ambao wataipa sapoti Uganda kutokana na kuondolewa kwa wachezaji wake 6 kwenye kikosi cha Stars kutokana na kuchelewa kufika kambini akieleza kuwa ni sababu ambayo haina maana.

Manara pia amefunguka kwa kusema sababu ya uwepo wa wachezaji wao Juuko Murushid na Emmanuel Okwi kwenye kikosi cha Uganda, isiwe sababu ya kuikacha Stars na badala yake akiwataka waweke utaifa mbele.

Mbali na kuipa hamasa Stars, Manara amewaomba mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho ambapo timu yao itakuwa inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya majira ya saa 12 jioni.

Sanjari na kujitokeza Uwanjani, mashabiki hao pia ambao watawahi watapata fursa ya kuutazama mchezo wa Uganda dhidi ya Stars ambao utarushwa mbashara kupitia kituo cha ZBC 2.

Share This Video


Download

  
Report form