Viongozi kutoka miungano tofauti ya wahudumu wa afya nchini wameikashifu wizara ya afya kwa kuingilia uongozi wao kwa kutoa pendekezo la kurekebisha sheria kadhaa za udhibiti wa maswala ya afya. Viongozi hao wakiwemo wa muungano wa madaktari nchini, muungano wa matabibu, muungano wa wauguzi na wengineo wamesema kuwa hawatokubali mtu yeyote kuingilia uongozi wao. Badala yake wameitaka wizara ya afya kuangazia maslahi yao wanapopambana na janga la corona nchini.