Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Ameliongoza Taifa Lake Katika Ibada Ya Wafu Ya Mwendazake Rais John Pombe Magufuli Katika Uwanja Wa Jamhuri Jijini Dodoma. Rais Hassan Ametumia Nafasi Hiyo Kuwapiga Vijembe Walio Na Shauku Kuhusu Uwezo Wake Wa Kuongoza Taifa Hilo Akisema Kuwa Yu Tayari Kuliongoza Taifa Baada Ya Kunolewa Vilivyo Na Hatati Rais Magufuli.