Waziri Wa Kawi Charles Keter Amepigwa Faini Ya Shillingi Laki Tano Kwa Kufeli Kufika Mbele Ya Kamati Ya Kawi Katika Bunge La Seneti.Keter Aliyekuwa Ameshurutishwa Kufika Mbele Ya Kamati Hiyo Inayoongozwa Na Seneta Wa Nyeri Ephraim Maina Kuelezea Sababu Zilizopelekea Kupandishwa Kwa Bei Ya Mafuta Alidinda Kwa Kutoa Sababu Ambazo Hazikuridhisha Kamati.Haya Yanajiri Wakati Kamati Ya Kitaifa Ya Hazina Ya Fedha Za Kustawi Maeneo Bunge Pia Ikionya Waziri Wa Fedha Ukur Yatani Kukosa Kufika Mbele Yake.Kamati Hiyo Inayoongozwa Na Mbunge Wa Kanduyi Wafula Wamunyinyi Imetoa Ilani Kwa Ukur Yattani Kufika Mbele Yake Juma Lijalo Kabla Ya Kuchukua Hatua Nyingine