Uamuzi Wa Mahakama Ya Kitaifa Ya Sheria Uliowafaa Taifa La Somalia Katika Mzozo Wa Mpaka Wa Baharini Unazidi Kuzua Mihemko Nchini. Rais Uhuru Kenyatta Kwa Mara Nyingine Ameshikilia Kuwa Kenya Haiko Tayari Kupoteza Mali Ya Wakenya Kupitia Uamuzi Wa Mahakama Ya Icj. Semi Zake Rais Unatarajiwa Kuchachawiza Mahusiano Baina Ya Somalia Na Kenya Huku Rais Akisema Kuwa Kenya Iko Tayari Kulinda Mipaka Yake Kwa Hali Na Mali.