Kamati Inayojukumika Na Uthibiti Wa Ukame Na Baa La Njaa Nchini Imesema Imeweka Mikakati Thabiti Ili Kuhakikisha Kaunti Zinazoathirika Na Njaa Zinapata Usaidizi Unaofaa Kwa Muda Ufaao. Kamati Hiyo Inayoongozwa Na Afisa Mkuu Mtendaji Wa Kampuni Ya Mawasaliano Nchini Peter Ndegwa, Imesema Inatarajia Kuchangisha Kima Cha Shilingi Bilioni Moja Ifikiapo Mwisho Wa Februari Na Pia Kutumia Kitengo Cha Wanajeshi Kuchimba Na Kukarabati Visima Vya Maji Ili Kuwanufaisha Wakenya Wanaokumbwa Na Uhaba Wa Chakula Na Maji.