Magoli yote: Simba SC 4-2 AFC Leopards (Mechi ya kirafiki - 08/09/2018)

Trend Video en 2018-09-09

Views 2

Timu ya soka ya Simba SC usiku wa leo Septemba 8, imepata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kujipima nguvu wakati ambapo ligi mbalimbali zimesimama kupisha michezo ya timu za taifa, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 14 mfungaji akiwa ni John Bocco.

Simba iliyotawala katika eneo la kiungo, ilipata bao la pili dakika ya 41 ambalo lilifungwa na Mohamed Ibrahim ambaye aliwachambua mabeki wa Leopards na kufunga kwa shuti kali.

Dakika ya 45, Leopards ilipata bao la kwanza mfungaji akiwa ni Eugen Mukangula ambaye alitumia vizuri makosa ya walinzi wa Simba katika kuokoa.

Dakika ya 57 Bocco aliifungia Simba bao la tatu na la pili kwake katika mchezo huo kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Mohammed Hussein.

Marcel Kaheza aliifungia Simba bao la nne dakika ya 79. Dakika ya 90 Ray Omondi aliipatia Leopards bao la pili.

Katika mchezo huu, AFC Leopards dakika ya sita ya mchezo na walitangulia kutikisa nyavu za Simba, lakini mwamuzi akaamua kuwa ilikuwa ni ‘off-side’. Je, wewe unaionaje?

Share This Video


Download

  
Report form