Imetimia mwaka mmoja tangu mkataba wa amani kati ya jamii zilizoko kwemye mpaka wa Kenya na Uganda ulipowekwa sahihi. Mkataba huo umepongezwa na wakaazi ambao wanaishi katika mpaka wa Kenya na Uganda kupitia kwa mradi kama vile ujenzi wa mabwawa. Kulingana na gavana wa Wespokot Professa John Lonyangapuo mkataba huo umepunguza visa vya ghasia ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa maeneo hayo kwa miezi kadhaa sasa.