Hamasa Kuhusu Bima Ya Nhif Imeendelea Katika Jiji La Nairobi, Hii Leo Ikielekezwa Katika Mtaa Wa Eastleigh. Wakaazi Walijitokeza Kwa Wingi Nakujisajili Ili Waweze Kupokea Matibabu Kwa Njia Ya Urahisi Katika Hospitali Za Umma Na Baadhi Ya Hospitali Za Kibinafsi Zinazowatibu Wakenya Kupitia Bima Ya Nhif. Bima Ya Nhif Inalenga Kufanikisha Mpango Wa Afya Kwa Wote Uliozinduliwa Na Serikali Ya Muhula Uliopita, Huku Kinamam Waja Wazito Wakinufaika Zaidi Na Bima Hii Afya.