Kundi La Pili Kutoka Lile La Mwisho La Wanafunzi Wa Darasa La Nane Kwenye Mtaala Wa 8-4-4 Waliofanya Mtihani Wa Kcpe Mwaka Jana, Hii Leo Wameanza Kujiunga Na Kidato Cha Kwanza Katika Shule Za Sekondari Mbalimbali. Wiki Hii Wanafunzi Zaidi Ya Laki Nane Wanatarajiwa Kujiunga Na Shule Za Upili, Pamoja Na Walimu Wapya 30,000 Walioajiriwa Na Tume Ya Kuajiri Walimu Nchini Tsc. Tayari Vitabu Vya Wanafunzi Hao Vimeshawasili Katika Shule Zote.