Jaji Mkuu Martha Koome Anasema Kuwa Serikali Haina Budi Ila Kuhakikisha Kuwa Idara Ya Mahakama Inapata Mgao Wake Kikamilifu Ili Wakenya Waweze Kupata Haki Kwa Wakati Mwafaka. Koome Ameyasema Haya Alipowaapisha Majaji Watakaohudumu Katika Korti Mpya Ya Madeni Madogo. Korti Hiyo Inatarajiwa Kukwamua Msongamano Wa Kesi Mahakamani Kwani Inasemekena Kuwa Idadi Kubwa Ya Kesi Zilizorundikana Mahakamani Ni Za Madeni Madogo