Katika Jitihada Za Kulinda Nyumba Na Hoteli Zilizoko Mkabala Na Ufuo Wa Bahari Hindi Ili Zisisombwe Na Maji, Serikali Ya Kaunti Ya Kilifi Imetenga Shilingi Milioni 73 Ili Kufadhili Ujenzi Wa Ukuta. Ukuta Huo Utajengwa Katika Eneo La Ngomeni Huko Magarini Kaunti Ya Kilifi Hasa Baada Ya Nyumba Kadhaa Kusombwa Na Maji Kufuatia Ongezeko La Maji Ya Baharini.