Rais Uhuru Kenyatta Ametoa Wito Kwa Mataifa Ya Kigeni Kutofunga Mipaka Yao Kutokana Na Aina Mpya Ya Corona Omicron. Akizungumza Katika Bunge Siku Ya Jumanne, Uhuru Alisihi Kwamba Mipaka Hiyo Iwachwe Wazi. Orodha Ndefu Ya Nchi Zimefunga Mipaka Yao Kwa Eneo Hilo Tangu Wanasayansi Wa Afrika Kusini Kutangaza Aina Mpya Ya Coronavirus Wiki Iliyopita. Kusimamishwa Ni Kwa Kuzingatia Uamuzi Wa Serikali Wa Kupiga Marufuku Kwa Muda Mawasiliano Ya Anga Kwenda Botswana, Eswatini, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini Na Zimbabwe, Ilisema Katika Taarifa. Wakati Huo Huo Aliwasihi Wakenya Kupokea Chanjo Ya Corona Ili Kupigana Na Aina Mpya Ya Corona Omicron.