Rais Uhuru Kenyatta amwewapongeza viongozi wanaoongoza mchakato wa kuleta amani katika taifa la South Sudan. Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa mataifa wanachama wa IGAD rais Kenyatta amesema kuwa hatua zilizopigwa katika muda wa miezi mitano sasa zitasaidia kuweka taifa hilo, lililogubikwa na vita tangu kujipatia Uhuru, mahala bora zaidi na kulisaidia kukua.